"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Ugandan Tracts

KUINUKA  na  KUANGUKA  kwa  HIMAYA

     Katika kumbukumbu za historia ya mwanadamu, kupangilia matukio na kuinuka na kuanguka kwa himaya, ni kitu kinachoonekana kuwa kinaamuriwa na utashi, nguvu, tamaa, na uwezo wa mwanadamu. Lakini katika neno la Mungu, pazia linaondolewa, na tunatazama kupitia mchezo wa kuinuka na kuanguka wa matukio ya mwanadamu, wakala Mmoja alieye na rehema, kwa uvumilivu akifanya kazi kutimiza mashauri ya mapenzi yake.
     Hakuna sehemu yoyote katika Maandiko kulipo na kanuni hii ikiwa imefunuliwa wazi zaidi kuliko katika sura ya pili ya Danieli. Hapa inaletwa machoni kwetu picha yote ya historia kuanzia wakati wa Danieli mpaka siku zetu za leo.

     Katika kipindi ambacho matukio haya yalikuwa yanatukia, mfalme Nebukadneza na ufalme wake wa Babeli ulitawala ulimwengu mzima wa wakati huo.
     Usiku mmoja mfalme alikuwa anashangaa juu ya kile ambacho kingefuata baadaye. Wakati akiangalia kwenye mji huu mkuu aliotawala juu yake, inaonekana kana kwamba ulikuwa hauonekani; na wakati huo hazikuwepo silaha [mashine] za vita za kuweza kubomoa kuta zake. Kuzunguka ukuta kulikuwa na shimo kubwa dhidi ya wavamizi lililofanywa na Mto Frati. Mto ulipita katikati ya mji, lakini kwenye sehemu ulipoingilia mjini, kulikuwa na malango makubwa yakienea hadi majini. Nyuma ya hayo malango zilikuwepo kuta zikizuia maji, kukiwa na malango ambayo yaliwezesha mtu kuingia mjini kwa njia ya mto. Malango haya yangefungwa imara kwa milango mikubwa ya shaba, kwa hiyo hata kama mtu angeweza kupita ng’ambo ya malango kwenye kuta hakukuwepo uwezekano wa kuingia mjini mpaka malango ya shaba yafunguliwe.


NDOTO YA MAANA SANA

     Wakati akitafakari mambo haya na akishangaa kama ufalme wake ungedumu milele, Nebukadneza alilala usingizi. Usiku ule alikuwa na ndoto ya maana, lakini alipoamka alikuwa hawezi kukumbuka kitu chochote. Alihisi hata hivyo, kuwa hii ndoto kwa namna fulani ilikuwa na majibu kwa swali lake juu ya mambo ya baadaye.
     Mara moja Nebukadneza aliwaita wenye hekima katika utawala wake kumsaidia akumbuke ndoto yake--haijalishi ni kiasi gani cha umizimu wao, unajimu, uchawi, au ulozi walihitaji kutumia. Wenye hekima walikusanywa, lakini hawakuweza, kupitia elimu ya mambo yote haya, kufunua ndoto ya mfalme. Akiwatambua hawa wenye hekima kuwa walikuwa wadanganyifu na kuwa wasingemsaidia, mfalme alikasirika na kuamuru wakamatwe na kuwekwa kizuizini wakisubiri kuuawa. Danieli na wenzake walidhaniwa kuwa wenye hekima, lakini hawakuitwa au kuwepo mbele ya mfalme. Hata hivyo, bado walijumuishwa katika kukamatwa wenye hekima kwa kijumla.
     Danieli alikata rufaa ili hatua hii ya kuuawa icheleweshwe, akiahidi kuwa baada ya muda mfupi angempatia mfalme habari alizokuwa anazitaka. Usiku ule yeye pamoja na wenzake waliweka ombi lao kwa bidii mbele za Mungu ili kujua ndoto ya mfalme na tafsiri yake. Walijua kwamba Mungu huwaheshimu wale wanaoweka tumaini lao lote kwake, na kwa hiyo walienda kulala wakiamini kwamba Mungu angefanya mapenzi yake yatimie. Usiku ule Mungu kwa rehema alifunua ndoto ya mfalme kwa Danieli, na hali kadhalika ilichomaanisha, hivyo ikionyesha kwamba Mungu pekee anajua ya mbeleni.


SURA YA SANAMU YA FALME

     Ndoto hii ya maana ilikuwa juu ya sanamu kubwa ambayo kichwa chake kilikuwa cha dhahabu. Kifua chake na mikono vilikuwa vya shaba. Miguu yake ilikuwa chuma, na nyayo zake na vidole vyake [pia] vilikuwa mchanganyiko wa chuma na udongo (angalia Danieli 2:28-33). Kichwa cha dhahabu kilitafsiriwa wazi wazi kuwakilisha Babeli (angalia Danieli 2:37-38). Chini ya Nebukadneza, Babeli ilikuwa imekusanya dhahabu kutoka katika mataifa yote iliyoyateka, [dhahabu hii] ikiifanya kuwa taifa tajiri sana la zamani.
     Lakini hiyo haiko katika ukuu wa utajiri unaodhaniwa, au katika hali ya kutoonekana ambayo mataifa au watu wanaweza kupata nguvu, bali katika kujua na kutimiza mapenzi ya Mungu. Na hatima yao inaamuriwa na mtizamo wao kwa makusudi ya Mungu kwao.
     Ufalme wa Nebukadneza uliishia tu wakati wa utawala wa mjukuu wake Belshaza, wakati taifa la pili, lililowakilishwa kwa kifua na mikono ya shaba, lilipongia katika uwanja wa kutawala. Kwa ujumla, ni ufalme ulio hodari zaidi ambao unashinda ule ulio dhaifu, lakini unabii unaonyesha kwamba hii isingekuwa utaratibu wa mambo (angalia Danieli 2:39). Katika sanamu, historia ya mataifa iliendelea kuanzia kwenye kichwa hadi kwenye miguu, na kila badiliko liliakisiwa kwa madini dhaifu yakilinganishwa na yale ya taifa lililotangulia.


BABELI YAANGUKA

     Majeshi shirikisho ya Waamedi na Waajemi yaliushambulia na kuushinda ufalme wa Babeli, kumwua Belshaza--mfalme wa mwisho wa Babeli, na kisha Dario Mmedi alitawala katika sehemu yake (Angalia Danieli 5:28-31).
     Zaidi ya karne moja kabla, Bwana alikuwa amefunua kupitia Isaya mbinu ambayo kwayo Babeli ingechukuliwa na mtu ambaye kupitia uongozi wake jambo hili lingetokea (angalia Isaya 44:27-28; 45:1-2). Chini ya uongozi wa Koreshi Mwajemi, majeshi ya Waamedi na Waajemi, yaliweza kubadilisha mkondo wa maji ya Mto Frati kwa muda kidogo. Wakati wa kipindi hiki waliingia mjini kwa kutumia njia ya maji ambayo waliyakausha. Hata juhudi zao zisingekuwa na maana, kama malango ya shaba yasingekuwa yameachwa wazi, bila kulindwa na walinzi wanaotetea [ufalme], wakati mfalme na wakuu wake walisherekea na kunywa (angalia Danieli 5).
     Kama tu fedha ilivyo dhaifu kwa dhahabu kithamani, basi Waamedi--Waajemi walikuwa dhaifu kwa utajiri na anasa. Wakati Himaya ya Waamedi--Waajemi ilikuwa na nguvu katika mambo ya vita na eneo walilokalia, haikuweza kuizidi Babeli katika kujilimbikizia utajiri au elimu. Himaya ya Waamedi/Waajemi ilikuwepo kwa karibu miaka mia mbili, kuanzia 539 KK hadi 331 KK.

     Ufalme uliofuata, ule wa shaba, ungewakilisha hatimaye ufalme ulioiangusha Uajemi. Tunajua kutokana na historia kwamba ilikuwa ni Wayunani, chini ya Alexander Mkuu, ambaye katika mapigano matatu ya nguvu (Granicus, mwaka 334 KK; Issus, mwaka 333 KK; na Arbela, mwaka 331 KK) aliyashinda majeshi ya Waajemi, akiifanya Uyunani Himaya ya baadaye. Ukweli huu wa kihistoria unaonyeshwa pia waziwazi katika njozi nyingine na Danieli, ulioko kwenye kumbukumbu katika sura ya 8, ambapo inaelezwa ufalme wa kuwashinda Waajemi ungekuwa Uyunani (angalia Danieli 8:2-8, 20-21). Shaba yalikuwa ni madini yaliyotumiwa na Wayunani kote, na pia yaliletwa katika utengenezaji wa silaha na vyombo vya vita.
     Roma, ambayo iliwakilishwa na miguu ya chuma, iliyashinda majeshi ya Kiyunani katika vita vya Pydna mwaka 168 KK. Roma hatimaye ilitawala ulimwengu kutoka mwaka 168 KK hadi 476 BK, wakati ilipoanguka mwishoni kwa makabila ya kivamizi ya washenzi.
     Kwa zaidi ya miaka 500, Roma ilionekana kuwa isingeshindwa. Bendera zake zilipepea kutoka visiwa vya Uingereza mpaka mto Frati, Kutoka Bahari ya Kaskazini mpaka Jangwa la Sahara. Makaisari wake waliabudiwa kama miungu, na kwa uwezo wake ilifanya ulimwengu wote kama nyumba moja ya kifungo. Katika maneno ya mwanahistoria Edward Gibbon, “Kupinga ilikuwa ni hatari ya kifo, na isingewezekana kuruka.” The Decline and Fall of the Roman Empire, gombo la 1, ukr. 190.
     Wakati Roma ilipoanguka, eneo lake liligawanywa katika sehemu kumi ambazo sasa zinafanya mataifa ya Ulaya. Kama ambavyo chuma na udongo kwa sehemu vina nguvu na kwa sehemu dhaifu, kwa hiyo ndivyo ingekuwa kwa mataifa haya kumi ya Ulaya ambayo nyayo na vidole vyake vya sanamu hii ilichowakilisha. Kama ambavyo chuma na udongo haviwezi kuchanganyika au kushikamana, kwa hiyo mataifa haya yenyewe yasingeungana kama dola ya mamlaka inayotawala ulimwengu.

     Kwa karne kumi na tatu za mwisho, watu wenye nguvu wametafuta kuhuisha utukufu wa Himaya ya Kirumi ya zamani, wakiunganisha pamoja mataifa mbalimbali ya Ulaya. Tukianza na Charlemagne na kuendelea na Charles V, Louis XIV, Napoleon, Kaiser William II, na Adolph Hitler--wote kwa ishara wameshindwa, japo kwa wakati lengo lilionekana kufikiwa. Maneno saba madogo ya unabii yalisimama katika njia yao: “Hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo” Danieli 2:43. Na mataifa ya Ulaya, moja moja au yote, hayatashikamana katika mamlaka ya kutawala ulimwengu tena!


NDOTO BADO HAIJATIMIZWA

     Lakini hii haikuwa mwisho wa ndoto. Pia ilifunuliwa kwamba katika siku za falme hizi, Mungu wa mbinguni atasimamisha Ufalme wake wa milele. Ufalme huu wa haki, uliowakilishwa na jiwe [mwamba] ambalo liligonga sanamu miguu yake, ungeendelea kukua mpaka dunia yote ijazwe, na hakuna hata mamlaka moja ya dunia ambayo ingezuia (angalia Danieli 2:34-35, 44).
     Ingawa wafalme wengi na mamlaka zimejaribu kumharibu Kristo--aliyewakilishwa na Jiwe (angalia 1 Wakorintho 10:4), na wameendesha vita dhidi ya wafuasi wa ufalme wa Kristo wa haki, bado hakuna hata [ufalme mmoja] uliofanikiwa na wala hakuna utakaofanikiwa. Kristo na ufalme wake utatawala milele, utukufu wake na kweli utafunika na kuijaza dunia hii kama tu maji yaijazavyo bahari (angalia Habakuki 2:14). Na mataifa yote maovu ya dunia yatasagwasagwa kama unga wakati Kristo--Mwamba anapokuja tena katika mawingu ya mbinguni.


BADO KUNA MUDA WA KUANGUKA KWENYE JIWE

     Rafiki, je utakuja kwa Kristo leo, ukianguka juu ya Mwamba huu wenye nguvu na kuvunjika katika moyo, ukitubu dhambi zako zote upate kuinuka na kuishi maisha mapya ukiwa na nafasi ya kuwa na uzima wa milele ikiwa utakuwa mwaminifu hadi mwisho? Au utabaki na majivuno na kutotubu, uking’ang’ania kwenye dhambi zako utakapokuwa umechelewa, na kukutikana na Mwamba huu wa nguvu ukikuangukia na kukusaga mpaka kuwa vumbi--bila nafasi ya uzima wa milele? Ndugu msomaji, je unataka kungukiwa na Mwamba huu mkuu na kupotea? Au unataka kupata hifadhi na kujificha katika Mwamba huu na kuokolewa? Uchaguzi ni wako.
     “Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu. Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye nguvu adui asinipate.” Zaburi 61:1-3.

     “Ingia ndani ya jabali; ukajifiche mavumbini mbele za utisho wa BWANA, mbele ya utukufu wa enzi yake.” Isaya 2:10.

     “Nimekukimbilia Wewe, BWANA, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye, uniopoe, Unitegee sikio lako, uniokoe. Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Nitakakokwenda siku zote. Umeamuru niokolewe, Ndiwe genge langu na ngome yangu.” Zaburi 71:1-3.

     “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.” Yohana 6:37.

Ili kupata habari zaidi juu ya mada hii muhimu, tafadhali bonyeza hapa