"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Ugandan Tracts

MNYAMA

     Mamlaka ya Mnyama wa Ufunuo 13:1-10 yameamsha hamu ya Wakristo kwa mamia ya miaka. Kumekuwepo uvumi wa aina nyingi kuhusiana na mnyama huyu, asili yake, na wakati atakapoonekana. Hitaji hili limewekwa vema, kwani Biblia inatoa onyo la nguvu juu ya mamlaka ya Mnyama huyu. Hata hivyo, uvumi siyo muhimu.
     Katika unabii wa Biblia, mamlaka za kisiasa mara ntingi zinawakilishwa na wanyama, au “Hayawani.” Mazoea haya hayafungwi na nyakati za Biblia, kwani bado tunatumia picha za wanyama kuwakilisha nchi leo. Hata hivyo, mwonekano wa Mnyama huyu pekee ni tofauti kutoka kwa mnyama yeyote tunayemjua na inaonekana ameumbwa na wanyama kadhaa tofauti wakiwa wamefanywa kitu kimoja. Hivyo, tunashindwa kumwita kwa jina la mnyama yeyote wa pekee, kama simba au dubu; na kwa hiyo amejulikana kwa kawaida kama Mnyama, au Mnyama mfano wa Chui, au Mnyama aliye na sura ya kutisha.
     Mnyama huyu ni wa kufurahisha sana kwa sababu anataka kuabudiwa kinyume na Mungu. Na ni kinyume na mfumo huu wa uongo wa ibada, pamoja na wale wanaoungana kama sehemu yake, ambao hasira ya Mungu, isiyochanganywa na rehema, inamwagwa (angalia Ufu 14:9-10).
     Katika kuangalia kwenye mistari ambayo inaongelea mamlaka haya, tunatambua kwamba kuna sifa nyingi au vigezo ambavyo vinasaidia kupambanua nani anamwakilisha. Kadiri tunavyochunguza kila dondoo ya hizi, inapaswa kuzidi kuwa wazi ni nani Mnyama huyu anapaswa kuwa.
     “Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba; yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lao la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule. Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wake wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila mabaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia.” Ufunuo 13:1-8.

     Watu wengi wanatazamia mamlaka mbaya ambayo italazimisha mambo yake katika uwanja wa kisiasa, ikiwalazimisha Wakristo kuacha imani yao kwa kuweka serikali isiyo ya kidini ya nguvu. Tunatakiwa kutambua, hata hivyo, kwamba kuna ibada inayoendana na mamlaka hii. Mstari wa 8 unasema kwamba watu wote duniani watamwabudu, isipokuwa tu wale ambao majina yao yako kwenye kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo. Na ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu kile cha uzima watakaookolewa! Yesu aliongea waziwazi wakati aliposema kuwa “Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.” Mathayo 7:14.
     Muda kidogo baadaye katika hubiri hilo hilo Yesu alitoa kauli nyingine ya kushangaza:
     “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.” Mathayo 7:21-23.

     Kutoka katika mafungu haya tunahitimisha kuwa wengi wa Wakristo waliopigwa bumbuazi hawatakuwa tayari kukutana na Kristo wakati arudipo. Kulingana na unabii, wote hawa watakuwa wanaabudu mamlaka ya Mnyama. Ukweli unapaswa kutuambia juu ya asili ya Mnyama huyu; kwa sababu kama mamlaka hii ingedai kuwa Mpinga Kristo, kama wengi wanavyotegemea, wachache sana katika ulimwengu wa Kikristo wangekutwa wakiiabudu.
     Kitu kinachofuata cha kuangalia ni kwamba Mnyama huyu ana mwili wa chui, na katika Danieli 7:6 taifa la Kiyunani lilikuwa linawakilishwa na chui (tafadhali tuandikie kwa ajili ya kipeperushi juu ya KUINUKA na KUANGUKA kwa HIMAYA). Watu wachache wanatambua ni jinsi gani falsafa za kipagani za Wayunani zimeteka kikamilifu ulimwengu, na pia zilifanya sehemu kubwa katika kuweka dhana ya kufikiri katika Kanisa.
     Wanafalsafa wachache wa Kiyunani wanajulikana kwa mvuto waliokuwa nao katika fikra za wanadamu. Wakati wa zama za giza, wakati Biblia ilipoharibiwa, watu walimwangalia Plato, Aristotle, na Socrates ili kupata nuru. Kama mmoja anavyoweza kutegemea, falsafa zao za kipagani kwa kiasi kikubwa zilipenyeza katika tafakari ya kidini, zikisaidia kujenga dhana zilizo nyingi ambazo zilikuwa sehemu ya imani ya Ukrisro, lakini ambazo hazikuwa na msingi katika Biblia.
     Kwa mfano; Plato aliamini katika roho kutokufa. Katika uelewa wake, mashujaa na watu mashuhuri walienda moja kwa moja katika makao na sehemu za kupewa tuzo, wakati watu wa kawaida walienda chini kuzimu kwenye mateso ili kupokea adhabu kwa unajisi wa dhambi mpaka ambapo wangekuwa wamesafishwa. Hapa tunaona imani ya kidini ya kuwainua watakatifu kwenda mbinguni baada ya kufa, na fundisho la purgatory (mahali pa kutakasa dhambi).
     Plato pia aliamini katika dhana ya kutenganisha mwili kutoka katika nafsi hai. Aliamini hili lingeweza kukamilika kwa kuutesa mwili, kwa kujinyima, na kwa kujitenga kutoka katika jamii. Hivyo, uliwekwa msingi kwa ujio wa ghafla wa imani ya kuishi katika sehemu za utawa na vitubio.
     Kitu kingine cha kuangalia ni kwamba Mnyama huyu alipanda kutoka kwenye maji ya bahari. Kulingana na Ufunuo 17:15, maji huwakilisha “jamaa na makutano na mataifa na lugha.” Kwa hiyo kile ambacho fungu hili linaeleza ni kwamba wakati mamlaka ya Mnyama huyu yalipotokea, yalipanda kutoka kwenye eneo ambalo lilikuwa limekaliwa na watu wengi--kama vile Ulaya, na siyo kutoka katika jangwa--au eneo ambalo lilikuwa na watu wachache.
     Ni muhimu kufahamu kwamba mamlaka ya Mnyama huyu yalikuwa pia yametabiriwa kuendelea kwa miezi 42, au miaka mitatu na nusu ya muda wa unabii. Tukitumia kalenda ya Kiyahudi ya siku 30 kwa kila mwezi, miezi 42 au miaka 3½ ingemaanisha siku 1260 za unabii. Katika unabii wa Biblia, kila siku moja ya muda wa unabii ingekuwa sawa na mwaka mmoja halisi wa muda (angalia Hesabu 14:34; Ezekieli 4:6). Hivyo, tunafahamu kwamba Mnyama huyu angetawala kwa siku 1260 za unabii au miaka halisi 1260.


Pembe Ndogo

     Katika Danieli 7, mamlaka hii hii ya Mnyama inafananishwa na Pembe Ndogo au ufalme ambao unang’oa na kuharibu pembe tatu au falme, na kisha kunena maneno makuu ya makufuru dhidi ya Mungu (angalia Danieli 7:8, 20-25). Mamlaka hii ingetawala “kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati” Danieli 7:25. “Wakati” huwakilisha mwaka mmoja katika unabii wa Biblia. Kwa hiyo mamlaka ya hii Pembe Ndogo ingetawala kwa wakati--au mwaka 1, nyakati--au miaka zaidi 2, na nusu wakati--au nusu ya mwaka. Hii ingeleta jumla ya miaka mitatu na nusu, au tena miezi 42 au siku za kiunabii 1260 au miaka halisi 1260. Hivyo, unabii wa Mnyama na mamlaka ya Pembe Ndogo inarejea kwenye mamlaka hii hii ya kidini.
     Wakati ambapo unabii wa aina hizi zote mbili unaonyesha kwamba mamlaka yaliyotambulishwa yangetawala kwa miaka halisi 1260, ni wakati gani kipindi hiki cha muda kilianza? Kitu kingine cha manufaa kinachoweza kutusaidia sisi kuthibitisha muda ambapo mamlaka hii ilianza, ni kwamba ingepewa kiti chake, uwezo wake, nguvu yake, na joka.
     Wakati joka huyu akirejewa kama Shetani (angalia Ufunuo 12:9), zaidi inalenga hasa kwenye Himaya ya Kirumi ya upagani wa zamani ambayo Shetani aliitumia kujaribu kumwua mtoto wa kiume--au Kristo--mara tu alipozaliwa (angalia Mathayo 2:1-18; Ufunuo 12:2-5). Kiti cha Himaya ya Kirumi ya zamani ulikuwa ni mji wa Roma wenyewe. Na kwa kuwa tarehe ya kuanguka kwa Himaya ya Kirumi ilikuwa 476 BK, iko wazi kwamba mamlaka hii ya Mnyama ingekuwa imeimarishwa thabiti pamoja na kiti chake na uwezo mpaka baada ya wakati huu.
     Kisha, mamlaka hii ya Mnyama ingekuwa ipi? Wakati Himaya ya Kirumi ilipoanguka, ufalme wake uligawanyika katika mataifa 10 ya kiserikali. Na ni mamlaka gani ya kidini ambayo iliinuka kutoka kwenye mabaki ya Roma ya Kipagani? Likidai vyeo [hadhi] na mamlka ya watawala watangulizi wake, Kanisa Katoliki taratibu lilitafuta kupanua mamlaka yake juu ya mataifa haya 10 ya kiserikali ya Ulaya. Mara moja watawala wa mataifa haya walipokea taji yao na kutawala zaidi au kidogo wakiwa chini ya mamlaka ya Kanisa Katoliki la Kirumi. Wakati baadhi wangedai kwamba upapa awali ya yote ni mamlaka ya kidini tu, tunapaswa kufahamu kuwa pia ni mamlka ya kisiasa ambayo hutuma na kupokea mabalozi na huendesha mambo kama serikali ya kisiasa.
     Kadiri ambavyo Kanisa Katoliki la Kirumi kwa taratibu lilipata mamlaka zaidi na utawala juu ya mataifa haya 10 ya kiserikali ya Ulaya, ilidhihirika wazi kwamba yote isipokuwa mataifa haya matatu (Heruli, Vandals, na Ostrogoths) yalipendelea, au yalijitoa kwa, mamlaka ya dini ya Kikatoliki. Kwa hiyo Kanisa Katoliki lilifanya vita dhidi ya mataifa haya matatu, na kuyang’oa kwa mfululizo (Heruli mwaka 493, Vandals mwaka 534, na Ostrogoths mwaka 538)--sawa kabisa na vile Biblia ilivyokuwa imetabiri juu ya haya mamlaka ya Mnyama wa Pembe Ndogo! Hivyo, mwaka 538 BK ungekuwa ndiyo kipindi cha kuanza kwa utawala wa Mnyama.
     Pia ilionyeshwa kwamba mwishoni mwa utawala huu wa Mnyama wa miaka 1260, mamlaka yake yangeondolewa, na ingepata jeraha ambalo lilionekana kuwa pigo la mauti. Lakini bado hili lingeponywa, na mamlaka hii hii tena ingeendesha uwezo wake juu ya wafalme wa dunia.
     Tukianzia na tarehe ya mwaka 538 BK, Kanisa katoliki lilitawala kwa miaka 1260 kabisa, na kisha likapokea jeraha la mauti mnamo mwaka 1798 BK. Majeshi ya Napoleon yalienda Ulaya yote, yakiangamiza tawala za kifalme na Kanisa. Jemadari wa Kifaransa Berthier, alishuka chini mpaka Roma na kumchukua Papa Pius VI akiwa mfungwa na kumpeleka Ufaransa kuishi miaka yake iliyobaki uhamishoni. Hivyo, Kanisa Katoliki lilikuwa, kwa kipindi cha muda, bila kichwa kinachoonekana cha kutawala. Hili lilikuwa kwa dhahiri ni pigo au jeraha la mauti kwa Kanisa, kwa sababu bila kichwa kinachoonekana au papa, Kanisa Katoliki lilikuwa limekufa! Lilikuwa limetawala kwa miaka 1260, na sasa lilikuwa halina nguvu--kama tu unabii ulivyotamka.
     Wengi waliamini kwamba Kanisa lilikuwa limefika mwisho na lisingeinuka kama sura tena ya manufaa katika mambo ya ulimwengu. Kwa miaka mingi picha hii ilibaki bila kubadilishwa, lakini mwaka 1929, Kardinali Gasparri na Benito Mussolini walitiliana saini mkataba uliorejesha mamlaka ya muda kwa upapa. Mara nyingine tena Vatican ilianza kufanya kazi kama ilivyowahi kufanya kabla.
     Hakuna yeyote anayeweza kuuliza kwamba tangu wakati huo upapa umerejesha heshima yake kubwa iliyopotea karne mbili zilizopita. Katika miaka ya 1950, wakati Harry Truman alipojaribu kuteua balozi rasmi kwenda Vatican, kuliamka upinzani ambao isingewezekana kwake kufuata alichokipanga. Lakini miaka 30 baadaye, wakati Rais Reagan alipojaribu kukamilisha jambo hili hili, alikumbana na upinzani mdogo.
     Jambo jingine la kukumbuka ni kwamba Mnyama huyu alikuwa na miguu ya dubu. Dubu katika Danieli 7:5 huwakilisha himaya ya Waamedi na Waajemi, na walikuwa na utaratibu wa serikali uliokuwa wao wa kipekee. Wakati mfalme wa Waamedi na waajemi alipotangaza sheria, alidhaniwa kuwa asiyeteleza (infallible). Mara sheria ikishatolewa, ilikuwa siyo rahisi kuibadilisha (angalia Danieli 6:8, 12, 15.) Hii inakuta hali ya kufanana katika fundisho la kutoanguka la papa wakati anapoongea zaidi ya hekalu, na kufafanua mada za sheria au mafundisho.
     Pia, katika kichwa cha Mnyama kulikuwa na jina la makufuru. Dhana ya Kibiblia ya makufuru inapatikana katika Marko 2. Viongozi wa Wayahudi walimshtaki Yesu juu ya makufuru kwa kudai haki ya kusamehe dhambi, haki iliyokuwa ya Mungu pekee (angalia mistari ya 5-7). Mamlaka haya ya Kanisa Katoliki pia hudai kuwa nayo.
     Jambo la mwisho kuangalia, ni kwamba unabii hutangaza kwamba mamlaka ya Mnyama huyu yangefanya vita na watakatifu wa Mungu. Hakuna ambaye ana maarifa ya historia anaweza kukataa kuwa maelezo haya, bila swali, yanastahili kwa Kanisa Katoliki la Kirumi. Inakadiriwa bila kubadilika kwamba Kanisa la Kirumi lilisababisha vifo vya watu zaidi ya milioni 50 katika kipindi chote cha utawala wake wa miaka 1260. Kwa nini watu hawa waliuawa? Kwa sababu walifuata ukweli wa Biblia na dhamiri zao--hata wakati zilipotofautiana na mafundisho yaliyoimarishwa na mamlaka ya Kanisa. Hivyo, iko wazi kwamba Mnyama wa Ufunuo 13:1-10 na Pembe Ndogo ya Danieli 7, bila makosa hurejea kwa Kanisa Katoliki la Kirumi!
     Wakati ambapo ni kweli kwamba uvumilivu kidini umeenea pote leo kuliko muda uliopita, unabii wa Biblia unasonda kwenye ukweli kwamba hii haitakuwa siku zote hivyo. Jeraha hili la mauti linegponywa kikamilifu, na mara moja Kanisa Katoliki lingepata tena mamlaka yake yaliyopotea. Kisha, sambamba na Makanisa yale ya Kiprotestanti ambayo yameungana na yanafanana nalo, watahuisha mateso ya nyuma dhidi ya wale wanaokataa kukubali na kuendana na mamlaka yao katika imani za kidini na matendo--wakichagua badala yake kufuata ukweli wa Biblia na dhamiri zao (angalia Ufunuo 13:15-17).
     Tunafahamu kwamba Mungu hakutoa unabii huu wa Biblia kama shtaka dhidi ya watu, lakini tu dhidi ya mifumo potofu ya kidini. Mungu amewatumia watu wake maonyo haya ya kinabii ili kusudi wasije wakahusishwa pasipo makosa katika upotovu huu wa Roma au katika Makanisa yoyote ya Uprotestanti ulioanguka ambayo yameunganika nalo.
     Katika Ufunuo 18, Mungu anarejea mifumo hii hii iliyopotoka ya dini kama Babeli. Katika siku hizi za mwisho tunakuta kwamba, kama vile tu Mungu alivyomwita Lutu kutoka katika Sodoma iliyopotoka na kujaa uovu kabla ya maangamivu yake, vivyo hivyo anatuma wito kwa watu wake leo wa “Tokeni kwake, enyi watu wangu”: kujitenga kutoka katika mifumo hii ya kidini ya uasi, “msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake” Ufunuo 18:4.
     Mungu anawaonya watu wake waziwazi wasijiunge na Makanisa yaliyopotoka au wasioamini, lakini wabaki wakiwa wamejitenga kutoka kwao wote. Kama wangeendelea kubaki wakiwa washiriki au wameshikamana na haya, hawatakuwa safi mbele za macho ya Mungu, hatawafikiria kama wana na binti zake, na watapoteza uzima wa milele (angalia 2 Kor 6:14-18; Isa 52:11; Mika 2:10).
     Ni kwa sababu upendo mkuu wa Mungu kwa wale ambao bado wameshikamana na hii mifumo ya kidini iliyopotoka; wengi wa wle ambao kwa dhati wanampenda kwa mioyo yao yote, kwamba anawaonya kuponyoka kutoka kwenye hatari dhahiri waliyomo. Kwa wema wake wa upendo na rehema zake za ukarimu Mungu anawaita watu wake kutoka katika Makanisa yote, ili waepuke maangamivu pamoja na Babeli, na badala yake washikamane na Kristo na ufalme wake wa haki, na hivyo kupata uzima wa milele.
     “Kimbieni kutoka katika nchi ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo…Enyi watu wangu; tokeni katikati yake, mkajiokoe nafsi zenu na hasira kali ya BWANA.” Yeremia 51:6, 45.